Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Kocha wa Dodoma Jiji fc Mbwana Makata amesema ushindi ulioipata timu yake leo dhidi ya Mwadui fc utakipa hamasa kikosi chake katika mikiki mikiki ya ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo Kocha Mbwana Makata amesema kikosi chake ni kigeni katika ligi hiyo hivyo ushindi huo utakipa nguvu na kijiamini katika ligi hiyo.
" Ushindi wa leo utakipatia confidence timu yangu kama unavyojua timu yangu ni ngeni kabisa kwenye ligi ingepoteza mchezo wa leo pia ingepoteza uwezo wa kijiamini katika ligi hii" amesema Makata.
Amesema timu yake imecheza vizuri sana kilichokosekena na maelewano tu kwa sababu imekaa pamoja kwa mda mfupi kabla ya ligi kuanza.
" Timu imecheza vizuri ila unganiko kwenye timu ndio ulikosekana ukiangalia nilianza na wageni saba lakini kadri mda ulivyokuwa ukienda nilianza kubadilisha kuingiza wenyeji ili kujenga maelewano na timu kucheza kitimu zaidi" amesema.
Amesema kikosi chake kipo imara kwa ajili ya mikiki mikiki ya ligi kuu na kadri siku zinavyoenda anaamini timu yake itaendelea kucheza vizuri sababu kikosi chake ni kizuri na kinawachezaji wazuri.
Kwa upande wake kocha wa Mwadui fc Khaleed Adam amesema timu yake imecheza vizuri makosa madogo madogo ndio yaliyopelekea kupoteza mchezo huo na anaamini michezo inayoendelea watafanya vizuri sababu timu yake anaiamini.
Mchezo huo ulikuwa mkali na wakusisimua kwani kila timu ilicheza vizuri huku timu ya Dodoma jiji ikishambulia mara kwa mara langoni mwa timu ya Mwadui fc hadi kipindi cha kwanza kinamalizika hakuna timu iliyokuwa imepata bao.
Bao pekee ya ushindi katika mchezo huo limefungwa na Khamis Mcha kipindi cha pili hivyo mpaka mwisho wa mchezo Dodoma jiji fc moja na Mwadui fc bila.

No comments:
Post a Comment