Search This Blog

Monday, September 14, 2020

Mahakama yamuukumu miaka miwili jela mwanamke aliejikata mkono ili alipwe na bima


Mahakama Jijini Ljubljana nchini Slovenia imemhukumu kifungo cha miaka miwili jela, mwanamke aliyejikata mkono wake wa kushoto akitarajia kulipwa zaidi ya £925,000 kama fidia ya matibabu kupitia mashirika ya bima.

Julija Adlesic mwenye umri wa miaka 22, alibainika kuwa alipanga na mpenzi wake kuukata mkono wake kwa makusudi wakiwa nyumbani kwao katika Jiji hilo, mapema mwaka 2019.

Baada ya uchunguzi wa kina, Adlesic alikutwa na hatia ya kujaribu kufanya udanganyifu ili kujipatia fedha kwenye mashirika ya bima, alikata bima za afya kwenye mashirika kadhaa mwaka mmoja kabla.

Kwa mujibu wa sheria za bima, endapo tukio hilo la kukata mkono lingeonekana ni halisi, angelipwa nusu ya kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya matibu punde tu baada ya kuripoti tukio, na kiasi kingine kingeendelea kulipwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...