Taarifa kuhusu kujisalimisha kwa magaidi hayo imetolewa na wizara ya mambo ya ndani ikifahamisha kuwa magaidi hao wamejisalimisha baada ya kuelemewa katika operesheni tofauti zilizoendeshwa na jeshi la Uturuki .
Jeshi la Uturuki limeendesha operesheni tofauti dhidi ya ugaidi katika maeneo tofauti katika mipaka ya Uturuki na Syria na Uturuki na Irak.
Taarifa hiyo iliotolewa na wizara ya mambo ya ndani ya Uturuki imefahamisha kuwa magaidi hao waliojisalimisha ni miongoni mwa magaidi waliojiunga na kundi la PKK miaka 6 iliopita mpakani mwa Uturuki na Irak.
Idadi ya magaidi ambao wamekwishajisalimisha kwa jeshi la Uturuki imefikia magaidi 144.

No comments:
Post a Comment