Search This Blog
Thursday, September 3, 2020
Kocha Mkuu wa Arsenal Afunguka Saini ya Aubameyang
MIKEL Arteta, Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa mshambuliaji wake namba moja Pierre Emerick Aubameyang atasaini dili jipya hivi karibuni.
Arteta ameongoza kikosi chake kutwaa mataji mawili kwa kuzinyoosha timu kubwa ikiwa ni pamoja na ule wa Kombe la FA ambapo aliichapa Chelsea mabao 2-1 na taji la Ngao ya Jamii alishinda kwa penalti 5-4 mbele ya Liverpool baada ya dakika 90 kutoka sare ya bao 1-1.
Mtupiaji wa mabao yote matatu alikuwa ni nahodha Aubameyang ambaye amekuwa akitajwa kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho.
Arteta amesema:"Nimekuwa nikisema jambo lilelile kuhusu Aubameyang. Ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kucheza michezo mikubwa.
"Nimekuwa nikipambana kuhakikisha namshawishi ili aweze kubaki kwenye timu hii naamini kuwa atakubali kusaini kwa kuwa hii ni timu yake bora na tukiwa pamoja tutafanya makubwa msimu ujao,".
Msimu mpya wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuanza Septemba 12 na mabingwa watetezi ni Liverpool.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment