Search This Blog

Saturday, September 12, 2020

CCM Biharamulo wazindua kampeni Mgombea ubunge atoa ahadi


Na Clavery Christian Biharamulo Kagera.

Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kimezindua kampeni zake rasmi wilayani humo kwa kuahidi kuendelea kuboresha miundombinu na kuboresha huduma za kijamii huku mgombea ubunge kupitia chama hicho akiahidi kutekeleza ilani ya chama chake na vipaumbele vyake vinne kwa wanabiharamulo.

Akizungumza katika uzinduzinwa kampeni hizo mgombea ubunge wa aliyechaguliwa na chama cha CCM wilaya ya Biharamulo Eng. Ezira John Chiweleza amesema kuwa endapo wananchibwa jimbo hilo watampatia ridhaa ya kuongoza jimbo hilo kwa miaka mitano atahakikisha anaboresha huduma za afya hasa upande wa kinamama wajawazito kwa kukaa na uongozi wa halimashauri ili waweze kuwaondolea michangobwanayolipa pindi wanapokwenda katika vituo vya afya na zahati kupata huduma ya afya zao.

Aidha amesema kuwa atahakikisha wanauongeza huduma za afya vijijini huku akiahidi kujenga uwanja wa michezo biharamulo ili kuweza kuboresha sekta ya michezo wilayani humo na kukuza vipaji vya vijana pamoja na kuanzisha biharamulo star search kwa vijana kila mwaka ili kuweza kutoa fursa kwa vijana wa biharamulo wanaotaka kujiajiri kupitia mziki. Eng. Ezira John amesema kuwa endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo ataajiri mwanasheria kwa ajiri ya kutatua matatizo ya kisheria kwa wananchi wa wilaya hiyo bure bila malipo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...