Search This Blog

Monday, September 28, 2020

CBT yatoa mafunzo na kuwaonya viongozi na watendaji wa AMCOS, wakulima na wasafirishaji


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Wakati uuzaji na ununuzi wa korosho ghafi kwa msimu wa 2020\2021 ukitarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Oktoba, mwaka huu. Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) imetoa angalizo kwa wakulima, vyama vya msingi vya ushirika(AMCOS) na wasafirishaji wawe makini ili kuepuka usumbufu utakaotokana kutozingitia ubora wa zao hilo.

Angalizo hilo limetolewa leo mjini Lindi na ofisa ubora wa korosho wa CBT, Joseph Merere wakati wa mafunzo ya siku moja ya uthibiti ubora wa korosho ghafi ngazi ya wakulima ambayo ilitolewa kwa watendaji na viongozi wa AMCOS zilizopo wilayani Lindi.

Merere alisema ili kulinda ubora wa korosho nakuwezesha ili zipate soko zuri na wakulima wauze kwa bei zenye tija kuna umuhimu na kila sababu ya wakulima, viongozi na watendaji wa AMCOS na wasafirishaji wazingatie ubora. Lakini pia  wataepuka matatizo yanayoweza kuwakuta kutokana na kutozingatia ubora wa zao hilo.

Alisema wakulima watakaopeleka maghalani korosho chafu ikiwamo zisizokauka vema watawajibika kwagharama zitakazohitajika ili kuboresha korosho zao kwa viwango vinavyohitajika. Lakini pia akionya kwamba wakulima watakaobainika kuweka vitu visivyokubalika ili kuongeza uzito korosho zao watawajibika kwamujibu wa sheria namba 18 ya mwaka 2009, kifungu cha 23(9).

Alibainisha kwamba  korosho zinatakiwa kuhifadhiwa sehemu kavu, isiyovuja na yenye hewa yakutosha. Kwani korosho zisipokaushwa vizuri zitaharibika, kuota au kuoza kabisa ndani muda mfupi tangu zihifadhiwe.

" Korosho zianikwe juani kwamuda wà siku tatu hadi nne mfululizo. Nivema korosho zianikwe kwenye sakafu nzuri, jamvi, vitanga, mikeka au maturubai. Korosho zilizokaushwa vizuri zina sauti kali inayosikika kama zitadondoshwa kwenye saruji au kuchezeshwa kwenye viganja," alisema Merere.

Hatahivyo Merere hakuishia kwa wakulima,bali aliwageukia viongozi na watendaji wa AMCOS kwakuwaonya kwamba  watakaopeleka korosho kwenye maghala makuu kwa ajili ya kuuzwa huku zikiwa hazijakidhi viwango vya ubora wajue kwamba hazitaondolewa na kupelekwa nje ya maghala hayo hadi ithibitike zimetoka chama gani. Ambapo viongozi na watendaji watawajibika kwa kubeba gharama zote zitakazo tokana na uzembe wao ili kuboresha korosho hizo.

"Viongozi na watendaji wa vyama vya msingi watakaogundulika kuruhusu, kusababisha au kuongezwa vitu ambavyo siyo korosho kwa nia ya kuongeza uzito na kupeleka maghalani kwa ajili ya mnada watawajibika kwamujibu wa sheria za nchi," alisisitiza Merere.

Katika hali iliyodhihirisha CBT imeamua kulivalia kibwebwe suala la ubora wa korosho, ofisa na mtendaji huyo aliwaonya pia wasafirishaji na wasindikizaji kutoka kwenye maghala ya vyama vya msingi kwenda maghala makuu  kwamba kukitokea upungufu wa uzito baina ya uliopimwa kwenye maghala hayo ya AMCOS na uzito utakao unaoonekana kwenye maghala makuu watawajibika kubeba hasara ya uzito utakao pungua.

Kwaupande wake mkaguzi mkuu wa ndani wa CBT , Ayubu Mumi ambae katika mafunzo hayo alimwakilisha mkurugenzi mkuu wa CBT alisema bodi ipo kwenye mchakato wa kuandaa mfumo rasmi wa uandaaji taarifa za usafirishaji na mapokezi ya zao hilo.

Alisema taairifa zisizo na mpangilio na utunzaji kumbukumbu usio sahihi zinachangia kuwepo changamoto zinazosababisha malalamiko toka kwa wakulima. Malalamiko ambayo yanasababishwa nakukosekana uadilifu kwabaadhi ya watendaji na viongozi wa AMCOS.

Nae makamo mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika cha Lindi Mwambao, Rashid Masoud alisema kukosekana uadilifu kwa baadhi ya viongozi na watendaji wa AMCOS  kunasababisha vyama vikuu na serikali kubebeshwa lawama.

Mafunzo hayo yaliandaliwa na kugharamiwa na CBT ambayo licha ya kuwezesha udhibiti ubora lakini pia yalilenga suala la maadili kwa watendaji na viongozi hao wa vyama vya msingi vya ushirika ambavyo mara nyingi vimekuwa vikilaumiwa kwa watendaji na viongozi wake wengi kukosa uadilifu na uaminifu.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...