Search This Blog

Sunday, September 13, 2020

Askari mmoja auawa katika shambulizi Hakkari


Wizara ya  mambo ya ndani ya Uturuki imefahamisha kwamba askari mmoja amefariki katika  shambulizi  la kigaidi lililoendeshwa na    magaidi  katika eneo la Hakkari.

Mkabiliano kati ya magaidi na wanajeshi wa Uturuki yalizuka baada  ya  magaidi kujaribu kuwavamia wanajeshi katika eneo hilo ambapo kumeanzishwa operesheni ya Yıldırım-1 Cilo.

Operesheni hiyo imeanzishwa na jeshi la Uturuki kwa lengo la kuwaondoa magaidi katika mipaka ya Uturuki kama ilivyoendeshwa operesheni nyingine mipakani mwa Uturuki.

Jeshi la Uturuki kwa uapande wake pia limefahamisha kuwaangamiza magaidi wawili .

Magaidi hao wameangamizwa wakiwa katika handaki lao ambalo  walikuwa wakitumia kama maficho Yüksekova.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...