Search This Blog
Tuesday, September 15, 2020
ACP Shana afariki dunia, Muhimbili waelezea
Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Jonathan Shana, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa akipatiwa matibabu.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital mapema leo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano hospitalini hapo Aminiel Aligaesha amethibitisha hilo na kusema kuwa marehemu alikaa hospitalini hapo kwa siku 21 na kati ya hizo alikaa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), kwa siku tatu.
"Jonathan Shana, Mstaafu RPC Mkoa wa Arusha amefariki usiku wa kuamkia leo Septemba 16, 2020, amelazwa hapa Muhimbili kwa siku 21, na kati ya siku hizo ICU amekaa siku 3", amesema Aligaesha.
Ikumbukwe kuwa Juni 24 mwaka huu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha ACP Shana kutoka kuwa RPC na kwenda kuwa afisa mnadhimu shule ya Polisi Moshi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment