Viongozi hao wa ngazi za juu nchini Uturuki wamewasili mjini Tripoli nchini Libya ikiwa ni katika ziara yao rasmi nchini humo katika kipindi ambacho kimepelekea hali ya vuta nikuvute kati ya Uturuki na mataifa kadhaa katika ukanda wa Mediterania .
Uturuki ilichukuwa uamuzi wa kushirikiana moja kwa moja na serikali ya Libya mabyo inatambulikana jumuiya ya kimataifa kupamabana na jeshi la jenerali mbabe wa kivita Khaftar.
Ziara hiyo ni baada ya kusainiwa makubaliano kuhusu usalama kati ya Uturuki na Libya.
Gwaride la heshima liliandaliwa katika uwanja wa ndege wa Mitiga kwa ajili ya kuwapokea viongozi hao katika jshi la Uturuki katika ziara yao.
Katika gwaride hilo , viongozi tofauti wa jeshi la Libya kama Selahaddin en-Numrush,Muhammed eshharif akiwemo pia balozi wa Uturuki mjini Tripoli wameshiriki katika hafla hiyo.

No comments:
Post a Comment