Viongozi waandamizi kutoka nchi za Afrika magharibi wamekutana na wanajeshi waliomwondoa madarakani rais Ibrahim Boubacar Keita.
Ujumbe huo pia ulikutana na rais huyo aliyepinduliwa. Juhudi za kusuluhisha zilianza kufanywa baada ya maalfu ya wananchi wa Mali kujitokeza katika mji mkuu Bamako ili kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na wanajeshi.
Viongozi hao kutoka nchi za jirani wanafanya mazungumzo kwa lengo la kuurejesha utawala wa kiraia nchini Mali.
Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS imelaani vikali kuangushwa kwa rais huyo na imesema itafanya juhudi ili kurejesha haraka utawala ulio katika msingi wa katiba na pia imesema inataka rais aliyepinduliwa Ibrahim Boubacar Keita arudishwe madarakani mara moja.
Jumuiya ya kimataifa pia imeleezea wasi wasi juu ya kuangushwa kwa rais Keita. Kiongozi wa ujumbe huo wa nchi za Afrika magharibi, Goodluck Jonathan aliyekuwa rais wa Nigeria amesema Keita anaendelea vizuri.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment