Search This Blog

Saturday, August 15, 2020

Vijiji vyote kupata umeme kupitia mradi wa ujazilizi

 Katika kuhakikisha vijiji vyote vinapata umeme hapa Nchini Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu amelitaka shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Morogoro kusimamia kikamilifu Mradi wa ujazilizi katika Kijiji cha Lumuma Wilayani Kilosa Mkoani humo.

Akiwa katika Kijiji Cha Lumuma kwenye hafla ya kuwasha na kizindua Mradi wa Umeme uliojengwa na TANESCO Mkoa wa Morogoro Naibu Waziri Mgalu amesema Serikali ya awamu ya tano inayongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli imefanya kazi kubwa ya kuhakikisha kila Kijiji hapa Nchini kinafikiwa na Nishti ya Umeme,ili wananchi wake waweze kutumia nishati hiyo katika kukuza uchumi.

Aidha, amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kupeleka Mradi wa ujazilizi katika Kijiji hicho ili wananchi wote wa kijiji hicho waweze kufikiwa na Nishati hiyo ,huku akisisitiza usimamizi mzuri kwa mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga Mradi huo

Katika hatua nyingine amesema upatikanaji wa Nishati ya Umeme katika Kijiji hicho kutainua uchumi wa Wilaya ya Kilosa, kwani kupitia Nishati hiyo kutawasaidia wananchi kuanzisha Viwanda vikubwa na vidogo vitakavyo saidia kukuza uchumi wa Kijiji na Wilaya kwa ujumla.

Aidha Mradi wa upelekaji umeme katika kijiji cha Lumuma ni kati ya Miradi inayotekelezwa na TANESCO Mkoa wa Morogoro kufuatia maelekezo ya Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subila Mgalu aliyoyatoa Mwezi 9,2019 alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kukagua maeneo ambayo hayana huduma ya umeme Wilayani Kilosa.

Hata hivyo, mradi huo umegharimu jumla ya 99,204,240.97 Fedha za Kitanzania, huku zaidi ya Wanajiji 238 wameunganishwa na huduma ya umeme kupitia Mradi huo,ambapo utawanufaisha katika matumizi mbalimbali ikiwemo katika Viwanda,Kilimo na Biashara mbalimbali.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...