Search This Blog
Sunday, August 16, 2020
Uchunguzi wa mlipuko Lebanon utachukua muda mrefu – Rais Michel Aoun
Rais Michel Aoun wa Lebanon amesema uchunguzi kuhusu mlipuko mkubwa uliotokea mapema mwezi huu mjini Beirut na kuwauwa watu 180 na kujeruhi maelfu wengine ni mgumu na huenda hautokamilika haraka.
Katika mahojiano na kiuto kimoja cha televisheni cha nchini Ufaransa, Auon amesema uchunguzi huo umegawanywa kwenye hatua tatu na utahitaji muda zaidi kuweza kubaini kikamilifu kilichotokea kabla ya kufikia hitimisho.
Akijibu kuhusu shinikizo la kumtaka kujiuzulu kutokana na madai ya uzembe, Aoun amesema suala hilo haliwezekani kwa sababu litaacha ombwe la uongozi nchini humo.
Hadi sasa chanzo cha moto uliozuka kwenye ghala lililohifadhi maelfu ya tani za milipuko katika bandari ya Beirut bado hakijulikani. Duru kutoka Lebanon zinasema viongozi wa juu wa nchi hiyo akiwemo rais Aoun walifahamu uwepo wa hifadhi hiyo ya milipuko lakini hawakuchukua hatua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Ujenzi, Arch. Elius Mwakalinga, akitoa maelekezo kwa Kai...

No comments:
Post a Comment