Search This Blog

Tuesday, August 18, 2020

Serikali yamaliza mgogoro wa ardhi kigamboni


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imemaliza mgogoro wa muda mrefu ulidumu kwa Miaka 20 katika eneo la vijibweni ambao wakazi zaidi ya 70 walikuwa na mgogoro na mwekezaji wa aliyefahamika kwa jina la Mkorea ambapo alinunua eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa Chuo Kikuu.


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni alikutana na wananchi hao katika kikao cha wazi na kufikisha maamuzi ya serikali kutokana na Mgogoro huo ambao katika kipindi chote hicho ulikuwa ukisababisha Vurugu na Uvunjifu wa Amani katika eneo hilo.


Katika Uamuzi wake Serikali kupitia Wizara ya Ardhi ilisema kuwa baadhi ya eneo hilo sasa litakuwa Chini ya Serikali na kutumika kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali, shule na Soko pamoja na Huduma nyingine za Kijamii.


Hata hivyo Uamuzi huo Ulipokelewa ndivyo sivyo na Wananchi hao huku baadhi yao wakionyesha wazi kukataa Fidia iliyotolewa na serikali lakini wengine wakisababisha Vurugu na maneno yasiofaa kwa Mkuu wa Wilaya na kusababisha baadhi yao kukamatwa.


Hata hivyo Bi. Msafiri aliwasihi wakazi hao kuwa hakutakuwa na Mabadiliko katika Maamuzi hayo ya Serikali kinyume chake waende Mahakamani ingawa hukumu ya awali ilionyesha kuwa wananchi hao waliuza na kulitoa kwa hiari yao eneo hilo kwa Mwekezaji.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...