Halid al Mashri, mkuu wa baraza kuu la Libya katika ziara yake nchini Uturuki amepokelewa na rais Recep Tayyıp Erdoğan mjini Istanbul.
Halid al Mashri amewasili Uturuki Alkhamis ambapo amefanya mazungumzo na rais Erdoğan na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Uturuki.
Katika mazungumzo yao , viongozi hao wa wamejadili kuhusu masuala tofauti kuhusu ushirikiano kati ya Uturuki na Libya.
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu amezungumza pia na Halid al Mashri.
Katika ujumbe wake aliotoa katika ukurasa wake wa Twitter, waziri wa mambo ya nje wa Uturuki amesema kwamba ushirikiano kati ya Uturuki na Libya unazidi kuimarika siku hadi siku.
Katika mazungumzo yao viongozi hao wamezungumzia pia kuhusu ushirikiano katika sekta ya uchumi na biashara na ulinzi.

No comments:
Post a Comment