Search This Blog

Thursday, August 6, 2020

Rais wa Poland Duda aapishwa kuongozwa kwa muhula wa pili


Rais wa Poland mhafidhina, Andrzej Duda ameapishwa kuongoza kwa muhula wa pili wa miaka mitano, lakini wabunge wengi wa upinzani na marais wa zamani na mawaziri wakuu wamejitega na utamaduni uliozoeleka na kususia sherehe hiyo. 

Viongozi wa kisiasa ambao hawakuhudhuria kuapishwa kwa Duda wakiwemo watangulizi Lech Walesa na Bronislaw Komorow waliashiria kile wanachokiona kuwa ni ukiukaji wa katiba ya Poland unaofanywa na Duda na kuzikubali sera za chama tawala cha siasa kali za mrengo wa kulia wakati wa muhula wake wa kwanza. 

Nyingi ya sera za chama cha Sheria na Haki zimeiweka Poland katika mgongano na Umoja wa Ulaya, ambao una wasiwasi kuwa juhudi za serikali za kuifanyia marekebisho idara ya mahakama na mambo mengine zimedhoofisha utawala wa sheria na demokrasia katika nchi hiyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...