Search This Blog
Saturday, August 1, 2020
Mwaga Mboga Tunamwaga Ugali..Ndege za Kenya zazuiwa kutua Tanzania
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesitisha kibali cha ndege za Kenya (KQ) kutua nchini rasmi kuanzia leo, Agosti 1.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Kenya kutoa orodha ya nchi ambazo raia wao wataruhusiwa kuingia nchini humo kwa ndege kuanzia leo watapofungua mipaka yao ya kimataifa.
Orodha hiyo haikuwataja Watanzania hivyo kupelekea Tanzania ambayo ilikuwa inaruhusu ndege za Kenya kuingia nchini kusitisha (nullify) ruhusa hiyo.
Ndege za Kenya hazitoruhusiwa kutua katika uwanja wa ndege wa JNIA – Dar es Salaam, KIA – Kilimanjaro, wala AAKIA – Zanzibar.
Kenya imetangaza kufungua anga lake kuanzia leo baada ya kulifunga kwa zaidi ya miezi minne ili kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment