Search This Blog

Sunday, August 23, 2020

Mke wa Alexi Navalny, amtembelea hospitalini mjini Berlin


Mke wa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexi Navalny, Yulia Navalnaya na maafisa wa juu nchini humo wamemtembelea kiongozi huyo hospitalini anakopatiwa matibabu mjini Berlin Ujerumani, baada ya kudhaniwa kupewa sumu. 

Navalny alisafirishwa kwa ndege kutoka Siberia hadi nchini Ujerumani baada ya madaktari kusema hali yake ilikuwa sawa kusafirishwa mjini Berlin katika hospitali ya Charite kwa matibabu zaidi. 

Baada ya kuwasili, msemaji wa hositali hiyo Manuela Zingl alisema kiongozi huyo wa upinzani aliye na miaka 44 atafanyiwa vipimo vya juu na madaktari hawatotoa taarifa zozote juu ya matibabu yake hadi watakapogundua kikamilifu matatizo ya mgonjwa wao.

 Navalny, mkosoaji mkubwa wa rais Vladimir Putin alilazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi siku ya alhamisi katika mji wa Siberia wa Omsk baada ya kuwa mgonjwa ghafla ndani ya ndege iliotoka Moscow kuelekea Siberia. 

Wafuasi wake wanaamini alipewa sumu na kwamba serikali ya Urusi ndio iliyohusika. Hata hivyo madaktari mjini Omsk wamekanusha madai ya Navalny kupewa sumu na kusema vipimo walivyomfanyia havikuonesha hilo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...