Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mgombea mtarajiwa wa ubunge katika jimbo la Lindi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amida Abdallah amehaidi kuanza na uboreshaji wa miundombinu ya elimu.
Amida ametoa ahadi hiyo leo mara baada ya kurudisha fomu za kugombea nafasi hiyo kwa msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya manispaa ya Lindi alipozungumza na wanachama na wapenzi wa CCM waliomsindikiza kurejesha fomu hizo.
Amida ambae ni mmoja wa wanawake wawili katika mkoa wa Lindi waliopitishwa na CCM kugombea ubunge majimboni alisema alikuwa na kiu kubwa ya ku boresha kiwango cha ufaulu wa katika jimbo hilo. Kwahiyo iwapo atafanikiwa kuchaguliwa ataanza na uboreshaji wa miundombinu ya elimu.
Alisema licha ya kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 lakini sekta ya elimu ni miongoni mwa sekta atakazo anza kushughulika nazo kwa kasi kubwa.
Amida aliyataja mambo mengine atakayoanza nayo kuwa ni mawasiliano, ujenzi na ajira. Huku akihaidi kushughulikia changamoto zilizopo katika jimbo hilo.
Aidha alitoa wito kwa wanachama na wapenzi wa chama hicho waungane nakuwa kitu kimoja ili chama hicho kipate ushindi mnono katika nafasi zote.
Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi wa halmashauri ya manispaa ya Lindi, Joomary Satura alisema hakuna mgombea atakae ondolewa bila sababu za msingi.
Isipokuwa atayethibitika ameshindwa kukidhi vigezo.
Alisema ofisi yake imedhamiria kutoa ushirikiano kwa wagombea wote katika hatua zote.
Alisema tume ya uchaguzi ina imani na wagombea wote. Kwahiyo wagombea watoe ushirikiano kwa tume na waiamini.
Mbali na Amida, wagombea wengine wa ubunge katika jimbo la Lindi ni Isihaka Mchinjita(ACT-Wazalendo), Mohamed Tahri(CHADEMA) na Salum Barwany (Chama Cha Wananchi-CUF).

No comments:
Post a Comment