Search This Blog

Thursday, August 6, 2020

Maandamano ya kupinga serikali yafanyika Lebanon

Waandamanaji katika mji wa Beirut walikabiliana na vikosi vya usalama vya Lebanon wakipinga serikali siku ya Alhamisi.

Maafisa wa usalama walirusha vitoza machozi kwa kundi la waandamanaji waliokuwa karibu na bunge.

Waandamanaji hao walikasirishwa na mlipuko uliotokea Jumanne, ambapo maafisa wanasema ulisababishwa na tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate ambazo zimekuwa zikihifadhiwa kwa njia isiyo sahihi tangu mwaka 2013.


Raia wengi wa Lebanon wanasema upuuzaji wa serikali ndio chanzo cha mlipuko huo, uliosababisha vifo vya watu karibu 137 na kujeruhi wengine 5,000.


Mlipuko huo uliharibu eneo zima la mji huo huku nyumba na biashara zikiharibiwa kabisa



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...