Search This Blog
Tuesday, August 18, 2020
Hiki ndicho kikwazo cha Guardiola kurejea Barca
Wakala wa kocha Pep Guardiola ,ajulikanaye kwa jina la Maria Orobitig amesema mteja wake hawezi kuondoka Manchester City kwa sasa na ataendela kusalia na kikosi hicho kutoka jiji la Manchester.
Guardiola anatajwa huenda akawa Kocha mpya wa FC Barcelona kuchukua Mikoba ya Kocha wa sasa Quique Setién ambaye huenda akafutwa kazi muda wowote baada ya timu hiyo kutolewa kwa kipigo cha aibu cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich kwenye mchezo wa robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Pep amewahi kuifundisha Baracelona kati ya mwaka 2008 mpaka 2012 na alikiongoza kikosi hicho kushinda mataji 14 ikiwemo ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya UEFA champions League mara mbili.
Josep Maria Orobitig amesema kwa asilimia mia moja mteja wake atasalia katika klabu ya Manchester city na atamaliza mkataba wa mwaka mmoja na Man City.
Makocha wengi wanaohusisha na Kibarua cha ukocha katika kikosi cha Barcelona ni Mauricio Pochettino, kiungo wa zamani wa kikosi hicho Xavi Hernandez,lakini hadi sasa taarifa zilizotufikia ni kwamba Ronald Koeman anakaribia kusaini mkataba wa kukifundisha kikosi hiko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment