Chama cha waandishi wa habari za michezo Mkoani Dodoma DOSWA leo kimepata safu mpya ya uongozi ambapo utakiongoza chama hicho kwa miaka miwili ijayo.
Mwenyekiti na msimamizi wa uchaguzi huo bwana Kim Rajabu ambaye ni mwamuzi mstaafu wa mpira wa miguu amemtangaza mwanahabari kutoka kituo cha radio Maisha Fm Rahim Shabani kuwa mwenyekiti wa chama hicho akipata kura 14 kati kura 17 zilizopigwa akimshinda mpinzani wake Virus Lukebo aliyepata kura 3.
Viongozi wengine waliochaguliwa ni Mwandishi wa BM Online Tv Timothy Francis ambaye amechaguliwa kuwa katibu wa DOSWA kwa kupata kura za ndio zote 17 ambapo hakuna kura iliyomkataa.
Mwandishi na mtangazaji wa Dodoma Fm Mindi Joseph yeye amechaguliwa kuwa muweka hazina wa chama hicho akipata kura 9 kati ya kura 17 akimshinda mwandishi wa magazeti ya New Habari Ramadhani Hasani aliyepata kura 8 kati ya 17 zilizopigwa.
Nafasi ya ujumbe wa chama hicho imechukuliwa na mwandishi wa gazeti la Majira Nuru Mkupa na mwandishi wa Dodoma Fm Matereka Jalilu nafasi ambazo wamezipata bila pingamizi kwa kuwa wagombea pekee.
Mara baada ya uchaguzi huo viongozi waliochaguliwa akiwamo mwenyekiti mpya wa DOSWA Rahim Shabani amesema amewashukuru wajumbe na kuahidi kufanya kazi kwa bidii na kuinua chama hicho na kufanya kazi usiku na mchana kusimamisha chama hicho.

No comments:
Post a Comment