Search This Blog

Sunday, July 19, 2020

Watanzania watakiwa kujenga tabia ya kusoma vitabu ili kuendana na uchumi wa kati

Na Clavery Christian Bukoba Kagera.


Katibu tawala wa mkoa Kagera Profesa Faustine Kamzola amesema kuwa kuna haja kubwa ya watanzania kujenga tabia ya kusoma vitabu mbalimbali ili kuweza kujiongezea kipato na kujifunza mambo mbalimbali kutokana na historia za watu na tafiti zinazo chapishwa katika vitabu vya siasa, uchumi, uongozi na historia za watu waliofanikiwa

Amesema hayo katika uzinduzi wa kitabu cha ''Siri ya binadamu kuishi miaka mingi Nguzo 72 zinazoshikilia Uhai Wako'' kitabu kilichoandaliwa na Mr Pius Ngeze mkurugenzi wa kampuni ya kuandika na kuchapisha vitabu mbalimbali ya TEPU HOUSE iliyopo Bukoba mjini ambapo amesema kuwa watanzania wengi hawapendi kujisomea na kusababisha ndoto na malengo yao kubaki chini na kusema kuwa ili nchi iweze kukua na kuendelea lazima watu wake wawe na tamaduni ya kujifunza.
 
 
Profesa Kamzola amesema kuwa watu wanaojiita wasomi inabidi kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii kuanzia kipato, akili ya utafutaji na ushauri kwa jami inayokuzunguka lakini lazima kuwa mtu wa kujifunza na kusoma vitabu vya watu waliofanikiwa kimaisha na kuishi miaka mingi bila kujali amesema au hakusoma ilimradi amefanikiwa kimaisha.

Kwa upande wake meneja wa kampun ya TEPU HOUSE amesema kitabu hicho kimelenga kuonyesha jinsi mwanadamu anavyozaliwa na kukua mpaka kufikia hatua ya uzee na hatimaye kufa ambapo amesema kuwa Mungu hajawai kuumba kiumbe kilicho dhaifu bali matatizo yanayojitokeza kwa baadhi wa watu yanasababishwa na malezi na utunzwaji wake kuanzia akiwa tumboni mwa mama yake mpaka kufikia hatua ya kuzaliwa na kulelewa mpaka kuwa mtu mzima na kujitambu kama vile uchumi duni wa familia, kushindwa kumcha Mungu na malezi mabaya ya watoto usababisha kiumbe huyu anayeitwa mwanadamu kuishi miaka michache hapa duniani tofauti na makusudio ya Mungu.

Mzee Piusi Ngeze ni mtunzi na mwandishi wa vitabu mbalimbali ambapo mpaka sasa ameandika vitabu 75 vyenye mafundisho mbalimbali ikiwemo vya siasa, uongozi bora, uchumi na historia za watu waliofanikiwa pamoja na adithi.
 
 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...