Search This Blog

Monday, July 13, 2020

Wapiganaji wa jihadi wawaua wanajeshi 10 wa Nigeria


Wanamgambo wa Kiislamu wamewapiga risasi na kuwaua wanajeshi 10 wa Nigeria Jumatatu kufuatia visa viwili tofauti katika eneo linalokumbwa na machafuko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Duru za kiusalama zimesema hayo na kuliambia shirika la habari kwamba wanamgambo hao walishambulia msafara wa wanajeshi karibu na kijiji cha Kumulla, takriban kilomita 40 kusini magharibi mwa mji mkuu wa jimbo la Maiduguri, na kuwaua wanajeshi wanane.

Wanajeshi wengine wawili waliuawa katika makabiliano tofauti na wanamgambo katika kijiji cha Kolore.

Mauaji hayo ya wanajeshi wa Nigeria yanajiri wiki moja tu baada ya wanamgambo ambao ni watiifu kwa kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS karibu na Kumulla kuwaua wanajeshi wengine 35.

 Kwa muongo mmoja wanamgambo wa Kiislamu wamekuwa wakifanya mashambulizi katika jimbo hilo na watu 36,000 wameuawa huku wengine milioni mbili wakilazimika kuyakimbia makaazi yao.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...