Search This Blog

Wednesday, July 8, 2020

Wananchi wa jimbo la Nanyamba wameshauriwa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yao




Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Wananchi wa jimbo la Nanyamba Halmashauri Mkaoni Mtwara wameshauriwa kuimarisha ulinzi shirikishi  na usalama katika maeneo yao ili kuepukana na matendo ya uvunjifu wa amani.

Wito huo umetolewa na mbunge wa Jimbo hilo Abdallah Dadi Chikota alipokuwa anazungumza na wananchi hao katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mnongodi ndani ya Halmashauri hiyo.

Chikota alisema kuwa na ni vyema kwa wananchi hao wakawa makini na wageni wanaoingia katika maeneo hayo kwani kijiji hiko kimekaribiana na vijiji vilivyopo nchi ya jiyani.

“Niwaombe wananchi wangu kwa sasa inatakiwa muimarishe ulinzi shirikishi wenyewe kwani suala hili la ulinzi linaanza na sisi wenyewe wanachi”Alisema chikota.

Chikota amekuwa mbunge wa kwanza toka kuanzishwa kwa Jimbo la Halmashauri ya Mji wa Nanyamba lilianzishwa mwaka 2015 kutoka kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...