Search This Blog
Tuesday, July 7, 2020
Waliotorokea Afrika Kusini warudishwa nchini
Watanzania 100 waliondoka nchini kinyume na sheria na kutokomea Afrika Kusini, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na shtaka la kuondoka nchini bila kufuata taratibu za uhamiaji.
Watuhumiwa hao ambao wengi wao wameonekana kuwa ni vijana, wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na wote wamekiri kutenda kosa hilo na wameiomba mahakama iwasamehe.
Hata hivyo, Hakimu Simba alisema kuwa haoni faida yoyote ya kuwapeleka watuhumiwa hao gerezani, hasa katika kipindi hiki ambacho kuna ugonjwa wa corona.
“Sioni faida yoyote ya kuwapeleka gerezani, lakini mahakama inawapa onyo kali na inawaachia kwa masharti msirudie kutenda kosa hili kwa miezi sita,” alisema Hakimu Simba.
Awali wakisomewa shtaka lao na wakili wa Serikali kutoka Uhamiaji. Godfrey Ngwijo, inadaiwa Julai 3, 2020 huko katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, washtakiwa wote 100 walikutwa wakiwa wameondoka nchini kinyume na sheria bila kufuata utaratibu wa kutoka na kuelekea Afrika Kusini.
Wakisomewa maelezo ya awali imedaiwa katika tarehe zisizojulikana washtakiwa hao waliondoka nchini bila kufuata utaratibu na kwamba Julai 3, mwaka huu walirudishwa nchini baada ya uchunguzi na kugundulika kuwa ni wahamiaji haramu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment