Search This Blog
Saturday, July 18, 2020
"Waliokosa amani nchini kwao wanakuja TZ" - Waziri mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewataka viongozi wa dini na Watanzania kwa ujumla kutumia nyumba za ibada kuhubiri suala la amani na utulivu.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu, katika Msikiti wa Buhari uliopo Ruangwa, mkoani Lindi, na kusema kuwa ni muhimu Watanzania wakajenga tabia ya kuaminiana, kuvumiliana pamoja na kupendana kwani mambo haya yote huchangia uwepo wa amani na utulivu.
"Nchi hii imejizolea sifa kuwa ni nchi ya amani na utulivu kwa sababu jambo hili linahubiriwa na viongozi wa dini zote, nchi hii sasa imekuwa ni kimbilio la nchi ambazo zimepoteza amani kwenye nchi zao, wanakuja hapa wanajifunza na wakirudi kwao wanaendelea kuwa salama" amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa ni jukumu la kila Mtanzania kuzingatia mahubiri ya viongozi wa dini ili nchi iendelee kuwa na amani kwani kukiwa na amani na utulivu lazima maendeleo yataonekana.
"Nchi yetu imekuwa na kasi ya maendeleo katika maeneo mengi, mimi naamini maendeleo haya yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na amani tuliyonayo na hii inatokana na mahubiri ya viongozi wetu wa dini, kwa kuwa dini ina mchango mkubwa sana katika uendeshaji wa Serikali".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment