Search This Blog

Wednesday, July 1, 2020

Vituo 7 vya TV vyapigwa rungu na TCRA


Kamati ya maudhui ya Mamlaka ya mawasiliano Tanzania - TCRA imevitoza faini vyombo mbalimbali vya habari jumla ya shilingi milioni 46 kutokana na kukiuka kanuni za mawasiliano ya kieletroniki na posta kuhusu maudhui ya utangazaji wa redio na Televisheni wa mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Makamu Mwenyekiti kamati hiyo ya maudhui TCRA Joseph Mapunda amesema makosa hayo yametokana na kurusha maudhui katika muda ambao watoto hawapaswi kuangalia ama kusikiliza, kutumia lugha isiyokuwa na staha yenye kudhalilisha kijinsia, maudhui yenye kukashfu utendaji wa serikali na viongozi, Maudhui yenye kushabikia mapenzi ya jinsia moja pamoja na kurusha maudhui bila kuweka mizania

Bwana Mapunda amesema licha ya kuvitoza faini vyombo hivyo pia imetoa onyo kali pamoja na baadhi ya vituo kutakiwa kuomba radhi kupitia vipindi vilivyobainika kutenda makosa hayo. Aidha katika kipindi cha mlipuko wa virusi vya corona kamati hiyo iliendelea kutekeleza majukumu yake ambapo ilivitoza faini baadhi ya vituo katika kipindi hicho.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...