UONGOZI wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2019/20 Simba umesema kuwa ,kiungo wao Luis Miquissone amezivutia timu nyingi nje ya nchi ambao wamekuwa wakiuliza kuhusu huduma ya nyota huyo.
Luis ambaye amebatizwa jina la Mmakonde amefunga jumla ya mabao matano kwenye ardhi ya Bongo katika mashindano yote ikiwa ni ndani ya ligi pamoja na Kombe la Shirikisho.
Ametupia mabao manne ndani ya ligi na pasi moja huku akiwa amefunga bao moja kwenye Kombe la Shirikisho, Julai 12 mbele ya Yanga.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa amekuwa akiuliziwa na marafiki zake kutoka Ulaya ambao ni mawakala kuhusu kumpata nyota huyo.
"Rafiki zangu watatu ambao ni mawakala wakubwa Ulaya wameshaniulizia kuhusu huyu Mmakonde, na tajiri nishamwambia, but (lakini) Simba inahitaji Quality players (wachezaji bora) kama hawa ili kufanya vema katika Champions league msimu ujao.(Ligi ya Mabingwa Afrika).
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment