Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Chama cha UDP kwa kauli moja imeamua chama hicho hakitasimamisha mgombea kwenye nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo chama hicho kimekubali kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa na Chama cha Mapinduzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutetea kiti hicho muhula wa pili
Julai 11 mkutano mkuu wa CCM ulimpitisha Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa asilimia 100 kuwa mgombea wa Urais.
Kamati kuu na halmashauri kuu ya UDP imekutana jijini Dodoma na kwa kauli moja wamekubaliana kuwa kwa kazi nzuri aliyoifanya Dkt. Magufuli hawaoni sababu yakusimamisha mgombea wa nafasi ya Urais katika chama chao.
Kwa maamuzi haya UDP wameungana na Chama cha TLP chini ya Mwenyekiti wao Augustino Mrema kilichokuwa cha Kwanza Kumuunga Mkono Rais Dkt. Magufuli.

No comments:
Post a Comment