Search This Blog

Sunday, July 19, 2020

Serikali kutafuta ufumbuzi bwawa la Kidete Wilaya ya Kilosa.


Bwawa la Kidete lililolalamikiwa na wananchi wa Kilosa Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli Wilayani humo limebainika kusababisha maafa ya watu 17 kwa mwaka huu pekee, kukata huduma ya maji safi ya kunywa pamoja na kuharibu na kusomba mazao ya wananchi wa eneo hilo la Kidete na kusababisha mafuriko katika mji wa Kilosa.

Mara baada ya wananchi hao kutoa malalamiko yao, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi aliyeambatana na Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba kwa lengo la kutekeleza agizo la Mhe. Rais Magufuli, amesema malalamiko ya wananchi wa Kidete ni dhahiri na yana mashiko baada ya kujionea mwenyewe na kuwaomba wananchi hao kuwa na subira wakati Serikali ikiangalia utaratibu wa kutatua kero hiyo.

Bwawa la Kidete lilijengwa na wakoloni wa kijerumani wakati wa ujenzi wa reli ya kati kwa lengo la kupunguza mafuriko kutoharibu miundombinu ya reli hiyo na liliharibika miaka ya 1990. Tangu wakati huo halijafanyiwa ukarabati jambo ambalo limesababisha maafa na adha kwa wananchi wa eneo la Kidete Wilayani Kilosa hadi pale wananchi hao walipolalamika kwa Mhe. Rais Dkt. Magufuli ambaye aliagiza ufuatiliaji wa kero hiyo ufanyike ili kuipatia ufumbuzi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...