Search This Blog
Tuesday, July 7, 2020
Serikali imetoa Sh.Bilioni 40 ujenzi wa vyuo vya VETA vipya 25.
Serikali imetoa sh.bilioni 40 ajili ya ukarabati na ujenzi wa vyuo vipya 25 vilivyojengwa katika Halmashauri tatu nchini.
Hayo ameyasema Meneja Uhusiano wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (VETA) Peter Sitta katika maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya sabasaba amesema tayari wilaya waandishi wa habari jana katika maonyesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya sabasaba amesema tayari wilaya tatu zimeshakamilisha ujenzi huo ambao ni Nkasi, Kasulu na Ileje.
Amesema ,kwa mwaka wa fedha ulioisha kulikuwa na miradi ya ujenzi na upanuzi wa vyuo 40.Sitta amesema lengo lao ni kuongeza udahili kutoka 704,000 hadi 1,000,000 kufikia mwaka 2020.
Hata hivyo Sitta amesema,lengo lao ni kuona wanafunzi wakiwa wabunifu wa kubuni vitu mbalimbali na kuweza kutatua changamoto za wananchi.
,Tunatambua maendeleo ya viwanda yanahitaji ujuzi na ubunifu ili kuwe na viwanda bora na vinavyozalisha bidhaa zinazotumika kwa wananchi kwa VETA kuwa suluhisho "amesema Sitta
Vilevile alisema, katika maonyesho hayo ya 44 wameleta teknolojia mpya 12 ambazo ni,kuzidua unga wa ubuyu,kuchemsha maji pasipotumia umeme,kuingiza umeme kwenye mita,ushonaji,kupanda mazao,ukaushaji wa samaki na teknolojia ya kuchenjua madini kutoka kwenye makenikia bila ya kutumia zebaki ambayo tayari imeshapigwa marufuku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment