Search This Blog

Wednesday, July 8, 2020

Penzi la Nandy na Bilnass Ngare Ngare....Bilnass Afikishwa Upareni Ukweni....


Baada ya kupita takribani miezi mitatu tangu Nandy kuvalishwa pete ya uchumba na Billnass sasa inaonekana wazi suala la ndoa linakaribia kwani wameonekana kufika ukweni kwa Nandy Usangi,Same mkoani Kilimanjaro.

Kupitia picha ambazo wamepost katika kurasa zao za mtandao wa kijamii wa Instagram inaonyesha kuwa Nandy amempeleka Billnass katika familia yake kwa kumkutanisha na Baba, Babu na bibi yake.

"Niko na mwenye jina lake Nandera bibi yangu kipenzi na babu yangu kipenzi upareni kwetu,   tuko na baba mzaa vyema na watoto wake Charles Mfinanga" ameandika Nandy

Aidha kwa upande wa msanii Billnass ameandika kuwa "Wapare ni watu wakarimu sana, na wenye upendo, sitamani kuondoka upareni, Usangi nimepapenda sana"

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...