Search This Blog

Wednesday, July 8, 2020

Mwanamke Shujaa aliyemuokoa Mtoto nyumba ikiwaka moto, mwenyewe afariki


Imewasikitisha wengi walioitazama ambapo pamoja na kuhuzunisha, Mwanamke huyu aliyemrusha mwanae kupitia kibarazani ametajwa na wengi kama shujaa, ni tukio la moto kuunguza nyumba gorofa ya tatu huko Phoenix, Arizona Marekani ambapo inaripotiwa ndani ya nyumba alikuwepo Mama na Mtoto na kwenye hii video Mama anaonekana akimuokoa Mtoto wake kwa kumrusha chini kupitia kibarazani.
Kwa mujibu wa ABC NEWS, Mama huyo alifariki kwakuwa alikua ameungua sana lakini alipambana na kuhakikisha amefika kibarazani na kumrusha Mtoto wake chini ambapo alidakwa na Watu wawili kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini, Mungu amlaze pema. (tahadhari video inaogofya)


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...