Search This Blog

Thursday, July 16, 2020

Mboya ashinda kura za maoni Moshi Mjini


Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Moshi, Raymond Mboya ameshinda kura za maoni za kuomba kuteuliwa kuwania ubunge wa Jimbo la Moshi Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mboya amechaguliwa na wajumbe wa chama hicho wa Mkutano Mkuu wa wilaya ya Moshi Mjini kwa kura 107 ambapo ni sawa na asilimia 70.9.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo, Ephata Nanyaro, alisema Mboya amekuwa mshindi katika uchaguzi huo na anategemewa kupeperusha bendera ya Chadema katika Jimbo la Moshi Mjini.
Aidha alisema wagombea wenza katika uchaguzi huo Ni, Antony Ndewawio  ambaye amepata kura kura 06 sawa na asilimia 3.6, Colince Mayuta  kura 10 sawa na asilimia 6.0Michael Kilawila kura 32 sawa na asilimia 19.4.
Akitoa shukrani zake kwa wajumbe hao, Raymond Mboya alisema amepewa jukumu kubwa la wananchi wa Moshi ya kuwaletea maendeleo na kwamba  atakuwa muaminifu katika shughuli zake zote za kisiasa pasipo kununuliwa.
“Maendeleo yanayoonekana kama reli, barabara na maeneo mengine yanamuhusu mheshimiwa rais hivyo maendeleo yaliopo hapa Moshi Mjini ikiwemo ujenzi wa stendi ya kisasa hapa yananihusu mimi na bado naahidi maendeleo makubwa zaidi, “alisema.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...