Majid Abdulkarim ,
Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima leo amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la mradi wa ujenzi wa hospitali mpya ya halmashauri ya Chalinze.
Hospitali hiyo ni kati ya 28 mpya zinazojengwa katika halmashauri mbalimbali nchini ambazo, mwishoni kwa mwaka wa fedha wa 2019/20 Serikali imetoa Tsh bilioni 14 kwa wastani wa Tsh milioni 500 kila moja ili kuanza ujenzi wa majengo mbalimbali.
Dkt Gwajima ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Pwani na Halmashauri ya Chalinze kwa kuanza vizuri na kutumia siku zao 14 za mandalizi ya uratibu wa ujenzi.
"Kwa sasa tayari eneo limeshasafishwa na vifaa vinapokelewa kesho kwa ajili ya kuanza ujenzi rasmi "Ameeleza Dkt Dorothy.
Aidha Dkt. Gwajima ameelekeza majengo ya awamu hii ya kwanza yakamilike ndani ya muda usiozidi miezi miwili.
Lakini pia Dkt Gwajima , amezitaka halmashauri zote zilizopokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa awamu hii kuweka ratiba ya kazi gani zitafanyika kila siku huku wataalamu wa afya wakiwa karibu na utekelezaji huo katika kila hatua na kutoa taarifa ya maendeleo kila baada ya siku saba.
Dkt Gwajima amesisitiza kuwa watakaokamilisha mapema na kwa ufanisi ndiyo watapewa fedha za awamu inayofuata ya mwaka 2020/21 na wasiokamilisha kwa wakati watakuwa na hoja ya kujibu na hatua stahiki zitachukuliwa.
Katika hatua nyingine Dkt Gwajima amewashukuru wananchi kwa ushirikiano wao kupitia Kamati za Uratibu wa ujenzi huu.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment