Search This Blog
Saturday, July 4, 2020
Godbless Lema Awaita Watia Nia Arusha Mjini
Aliyekuwa mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Godbless Lema amefurahia watu wengi zaidi kujitokeza kuweka nia ya kugombea ubunge kwenye majimbo mbalimbali ikiwemo kwenye lililokuwa jimbo lake Arusha Mjini.
Lema ambaya bado hajatangaza nia ya kugombea ubunge amewataka watu kujitokeza kwa wingi zaidi na kuacha uoga.
“Nimefarijika jinsi watu wanavyo chukua hatua ya kugombea ubunge na udiwani.Manyara, Tanga, Arusha na Kilimanjaro, tutapigana kufa na kupona ktk uchaguzi,tuendelee kuimarika ktk haki kwamba kesho ni nzuri sana. Twendeni mpaka mwanzo wa bahari. Msiogope” ameandika Lema kwenye ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa Twitter.
Kauli ya Lema inakuja ikiwa ni takribani wiki kadhaa zinasubiliwa ili wanachama waweze kuchukua fomu kwenye majimbo kwa ajili ya kuomba kuteuliwa na vyama vyao husika kugombea nafasi mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment