Wajumbe wa UWT Mkoa wa Mtwara siku ya jana walipata fursa ya kuwachagua wananchama ambao watakaoweza kuwa wabunge wa viti maalum wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mtwara mara baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu mwezi oktoba 2020.
Katika uchaguzi huo Agness Hokoro ameongoza kwa kupata kura 305,nafasi ya pili imekamatwa na Athmin Mapililo kwa kupata kura 255,nafasi ya tatu imekamatwa na Daisy Ibrahim kwa kupata kura 193 na Annastadhia Wambura ambae aliyekuwa Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Mtwara ameshika nafasi ya Nne kwa kupata kura 125.
Jumla ya wanachama 36 waliokuwa kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuwania Ubunge maalum kwa mkoa Mtwara huku Makao Makuu ya Chama ndio wenye jukumu la kuamua ni nani atapewa nafasi mara baada ya vikao kufanyika.
Msimaminzin wa uchaguzi huo ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gellasius Byakwanwa amesihii wagombea hao kuendelea kushikamana kwa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Octoba 2020.
Wajumbe waliotakiwa kupiga kura waliotakiwa kupiga ni 489 ila waliopata nafasi ha kupiga kura walikuwa 471 kati ya kura hizo kura 1 iliharibika.

No comments:
Post a Comment