Search This Blog
Wednesday, July 29, 2020
Agizo la Rais Uwanja wa Mkapa laanza kutekelezwa
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imeanza kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kubadili jina la uwanja wa Taifa kumuenzi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamini Wiliam Mkapa.
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo imeanza kutekeleza maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli kubadili jina la uwanja wa Taifa kumuenzi Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamini Wiliam Mkapa.
Taarifa hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Yusufu Singo, na kueleza kuwa mchakato umeshaanza na wameshaliondoa jina la zamani ili kuweka jina la Benjamini Mkapa, kwa maelekezo ya Waziri wa Michezo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
'' Baada ya maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt John Pombe Magufuli kutaka uwanja huu ubadilike ili tuweze kumuenzi Rais wa awamu ya Tatu, Hayati Benjamini Mkapa, tayari Waziri mwenye dhamana ya michezo na katibu Mkuu wa Wizara ya michezo, wameelekeza tuanze shughuli hiyo mara moja na tumeanza kuliondoa jina la zamani la 'National Stadium.'' Alisema Singo.
Singo ameongeza kuwa baada ya kuliondoa jina la zamani la uwanja huo, lakini kuna changamoto kidogo ya kuliweka jina jipya hivyo wanasubiri kukutana na wataalam wa Wizara, huku mafundi wakiwa tayari wanaendelea na ujenzi kwenye eneo husika.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Pombe Magufuli alitoa maelekezo ya kubadili jina la uwanja wa Taifa, uitwe Uwanja wa Benjamini Mkapa, wakati akitoa salamu za rambirambi kwenye kuuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamini Wiliam Mkapa, Jumanne hii kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment