Search This Blog
Thursday, June 25, 2020
Yanga yazungumzia sakata la Tshishimbi kugoma
Klabu ya soka ya Yanga imekanusha taarifa zinazoenea juu ya nahodha wake Papy Tshishimbi kuwa amegoma kuichezea miamba hiyo kwa sababu za madai ya maslahi yake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu hiyo, Hersi Said ameiambia Kipenga kwamba Tshishimbi bado anauguza jeraha linalomkabili na ameanza mazoezi mepesi na si kama inavyoripotiwa.
Kuhusu Mohamed Banka anayeripotiwa kuwa amerejea kwao visiwani Zanzibar akishinikiza malipo yake, Hersi Said amesema hana taarifa juu ya mchezaji huyo ingawa hadai mshahara labda pesa za usajili.
Katika hatua nyingine Hersi amesema kwamba wameshakamilisha mikakati ya usajili kabambe wenye tija utakaoisaidia timu hiyo kurejesha hadhi yake ya kutwaa mataji.
Vilevile amesema upo uwezekano wa Yanga kucheza na Sevilla ya Hispania Katika kilele cha wiki ya mwananchi kwa kuwa tayari wameshaingia makubaliano ya ushirikiano Katika nyanja mbalimbali ya kimichezo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment