Search This Blog

Monday, June 15, 2020

Wanaokatisha masomo mabinti kuchukuliwa hatua


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kuchukua hatua kali kwa watu wote watakaothibitika kufanya vitendo vya kuwakatisha watoto wa kike ndoto za masomo ikiwemo kuwafunga jela miaka 30.

Pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote nchini wahakikishe wanaendelea kushirikiana na Kamati za Ulinzi na Usalama hadi ngazi za kata kusimamia Sheria ya Elimu ya kuwalinda watoto wote wa kike walio chini ya umri wa miaka 18.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati alipoweka Jiwe la Msingi na kukabidhiwa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Bunge High School iliyojengwa na Wabunge katika Kata ya Kikombo jijini Dodoma kwa thamani ya zaidi ya tsh. bilioni moja.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...