Search This Blog

Tuesday, June 23, 2020

Trump na Macron waijadili Libya


Rais wa Marekani Donald Trump amefanya mazungumzo na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuhusu hali inayoendelea Libya.

Trump amependekeza kusitishwa kwa mapigano nchini humo haraka iwezekanavyo.

Kulingana na taarifa kutoka ikulu ya rais nchini Marekani, viongozi hao wawili walisisitiza kwamba lazima kusitisha mapigano nchini Libya na kwamba mazungumzo kati ya pande mbili yanapaswa kufanyika.

 Trump na Macron wamesisitiza kwamba zoezi la kuongeza wanajeshi kwa pande zote lazima kusitishwe haraka iwezekanavyo kuzuia mzozo kuwa hatari zaidi nchini Libya.

Viongozi hao wamezungumza kwa njia ya simu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...