Search This Blog
Thursday, June 11, 2020
Trump apongeza polisi ya Marekani, apuuza kilio cha waandamanji kuhusu ubaguzi
Rais Donald Trump wa Marekani amelipongeza jeshi la polisi nchini humo huku akipuuzilia mbali kilio cha waandamanaji ambao wanasema kuna ubaguzi mkubwa katika jeshi hilo.
Trump ameyasema hayo Alhamisi huku maandamano yakiendelea nchini Marekani baada ya polisi mzungu mbaguzi kumuua kinyama Mmarekani mwenye asili ya Afrika.
Mnamo Mei 25, afisa wa polisi katika mji wa Minneapolis jimboni Minnesta nchini Marekani alimbinya shingo kwa kutumia goti kwa dakika 9 hivi George Floyd, Mmarekani mweusi mwenye asili ya Afrika hadi akakata roho.
Mauaji hayo ya kinyama yaliibua maandamano makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa Marekani kupinga ubaguzi wa rangi huku miito ikitolewa ya kulifanyia marekebisho jeshi la polisi nchini humo.
Katika hotuba yake jana, Trump amedai kuwa ni maafisa wachache wabaya katika jeshi la polisi. Hadi sasa Trump amekataa kuzungumza wazi wazi kuhusu ukatili wa polisi dhidi ya Wamarekani weusi huki akidai kuwa maudhui hiyo si muhimu.
Hayo yanajiri wakati ambao sanamu zinazoashiria ubaguzi zimeangushwa, kuharibiwa ama kuondolewa na waandamanaji katika maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na sanamu la Christopher Columbus mjini Boston na sanamu ya Edward Colston aliyekuwa mfanyabiashara wa watumwa, katika karne ya 17.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment