Search This Blog
Wednesday, June 10, 2020
Sisitizo la Borell la kuondoka Marekani JCPOA na madai yasiyo na msingi ya serikali ya Trump
Rais Donald Trump wa Marekani ni mmoja wa wapinzani wakubwa wa mapatano ya nyuklia ya Iran yanayojulikana kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na ambaye aliitoa nchi hiyo katika mapatano hayo ya kimataifa tarehe 8 mwezi Mei 2018.
Pamoja na hayo lakini kila mara anapoona maslahi yake yakiwa mkwenye mapatano hayo huanza kudai kuwa ana haki ya kunufaika nayo, kama tunavyoshuhudia hivi sasa ambapo anadai kuwa ana haki ya kuchangia kurefushwa vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Msimamo huo wa Trump unapingwa na kundi la 4+1 ambalo linazijumuisha nchi za Magharibi na Mashariki wakiwemo wanachama wa kudumu wa Baraza la Uslama la Umoja wa Mataifa. Katika uwanja huo, Joseph Borell, Mkuu wa Siasa za Nje wa Umoja wa Ulaya alisema siku ya Jumanne kuwa Marekani tayari imejitoa katika mapatano ya JCPOA na kwa hivyo haiwezi tena kunufaika na haki zake za uanachama katika mapatano hayo kujaribu kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran. Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na Wang Yi Waziri wa Mambo ya Nje wa China na kusisitiza kuwa Marekani haina tena nafasi yoyote katika mapatano hayo. Amesema: Marekani tayari ilijiondoa katika JCPOA hivyo haiwezi kudai kuwa ni mwanachama wake ili iweze kunufaika na uanachama huo katika kuiwekea Iran vikwazo vya silaha. Ni wazi kuwa tayari walijitoa JCPOA.
Upinzani wa viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Ulaya dhidi ya madai ya serikali ya Donald Trump ya kuwa na haki ya kunufaika na mapatano ya JCPOA unaonyesha wazi kwamba hata washirika wakubwa wa marekani barani Ulaya nao pia wanayachukulia madai hayo kuwa dhaifu na yasiyo na msingi wowote. Borell amesema wazi kwamba Marekani ilijiondoa katika mapatano ya JCPOA mwezi Mei 2018 na kwamba tokea wakati huo haijawahi kushiriki katika vikao muhimu vya mapatano hayo ambavyo vimekuwa vikiandaliwa na Kamisheni ya JCPOA. Hii ni katika hali ambayo Marekani inadai kuwa bado ni mshiriki wa mapatano hayo ya kimataifa na hivyo ina haki ya kunufaika na haki za uanachama katika kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.
Baada ya kushindwa madai yake hayo, Marekani katika hatua ya pili inadai kwamba kwa kuwa ilikuwa moja ya nchi zilizoshiriki katika kupitisha azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama hivyo ina kila sababu ya kunufaika na haki ya ushiriki huo. Hoja dhaifu na zisizo na msingi za viongozi wa Marekani kuhusu suala hilo zinathibitisha wazi kwamba msimamo wa serikali ya Trump hauna msingi wowote wa kimantiki katika uwanja huo.
Siasa zinazotekelezwa hivi sasa na serikali ya Trump kwa ajili ya kurefushwa muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kutoa mashinikizo dhidi ya Baraza la Usalama ili lisalimu amri na kukubali kutekeleza matakwa haramu na yasiyo ya kisheria ya utawala wa Washington. Brian Hook, mwakilishi wa Marekani katika masuala ya Iran ameelezea wasiwasi wake kuhusiana na kukaribia kumalizika muda wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran hapo mwezi Oktoba mwaka huu na kusema iwapo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halitarefusha vikwazo hivyo, basi Washington itatumia mbinu nyingine kufikia lengo hilo. Huku akidai kuwa pendekezo la kuondolewa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran ni kosa kubwa lililofanyika katika mapatano ya JCPOA, Mike Pompeo, Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani amesema kuwa Washington inafanya juhudi zote ili kurefushwa vikwazo hivyo kupitia Baraza la Usalama. Ameendelea kusema kuwa Washington ina hamu kubwa ya wanachama wote waliopitisha azimio nambari 2231 washiriki kwa pamoja katika kurefusha vikwazo vya silaha dhidi ya Iran na kusisitiza kwa kusema: Iwapo hilo halitatimia, tutatumia uwezo wetu wa kidiplomasia kufikia lengo hilo. Jambo hili ni muhimu sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment