Search This Blog

Saturday, June 20, 2020

Simba na Mwadui kuvaana leo


LEO Uwanja wa Taifa, Simba itawakaribisha Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa majira ya saa 10:00 jioni.

Simba itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Juni 14 huku Mwadui FC wakiwa wametoka kupoteza mchezo wao mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Kambarage.

Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wapo tayari kuvaana na Mwadui kwa kuwa makosa yao wameyafanyia kazi.

"Makosa ya mchezo wetu uliopita dhidi ya Ruvu Shooting tumeyafanyia kazi, tuna amini tutapata matokeo mbele ya Mwadui FC kwani malengo yetu ni kupata matokeo chanya," amesema.

David Chakala, Meneja Mkuu wa Mwadui FC amesema kuwa benchi la ufundi limejipanga kuona nao wanapata pointi tatu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri.

Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 72 huku Mwadui FC ikiwa nafasi ya 12 ikiwa na pointi 34 zote zimecheza mechi 29.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Kambarage Simba ilinyooshwa bao 1-0 zama zile ikiwa chini ya Patrick Aussems.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...