Search This Blog

Monday, June 8, 2020

Mozizi, Tuisila nao waliamsha mapema

By MWANDISHI WETU

ACHANA na matokeo ya mechi yao ya kirafiki ya jana waliyopigwa 3-0 dhidi ya KMC, si unajua Yanga imekuwa ikihusishwa na orodha ya mastraika wanaotajwa kusakwa Jangwani, sasa unaambiwa yuko mmoja tu ambaye ana sifa zilizowachanganya mabosi wa klabu hiyo, Mpiana Mozizi. Jamaa huyo buana amefichua Mambo mawili mazito, huku ikielezwa tayari ameliamsha mapema nchini DR Congo sambamba na winga aliyemtaja kama moto mkali, Tuisila Kisinda ili kujiweka fiti mapema.

Ipo hivi. Matajiri wa Yanga, wameuma meno wakipania kufanya usajili mzito ndani ya klabu hiyo na kupitia Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Mhandisi Hersi Said ametamba kwamba katika usajili wao ujao watachukua washambuliaji bora wanaoongoza na kuwa wafungaji bora lakini pia watachukua winga mkali kutoka klabu bora Afrika.

Wakati kauli hiyo inatoka, mmoja wa washambuliaji ambao wanatajwa kuchukuliwa na Yanga ni Mpiana Mozizi alisema ana uhakika kwamba msimu ujao atacheza Yanga na kujiandaa na hilo amemtafuta winga Tuisila Kisinda wakianza kujifua mapema.

Mozizi ameliambia Mwanaspoti jana kutoka Congo, kwamba kama kuna kitu amekikubali ni hesabu za Yanga kumtaka Kisinda kwani ni winga ambaye amekuwa akitamani kucheza naye kutokana na ujuzi wake wa kujua kutengeneza nafasi.

“Niliambiwa na bosi wangu kwamba wanamchukua na Tuisila, nikaona ni jinsi gani Yanga wanataka kutengeneza timu bora, Tuisila ni winga mzuri anayejua,” alisema Mozizi.

“Namjua sana Tuisila ni winga bora hapa Congo ukicheza naye kama mshambuliaji unakuwa ba uhakika na kile ambacho anakitengeneza.

Advertisement

Mozizi alisema ameamua kufanya naye mazoezi winga huyo wa AS Vita kutokana na kutamani kuzoeana naye mapema lakini pia kujiandaa vyema.

“Nafanya naye mazoezi kwasasa tuna kama siku ya nne tunafanya pamoja, ni vizuri kujiandaa hapa ligi imekatishwa haitaendelea kabisa sasa ni bora tukawa na mazoezi binafsi kwa kipindi hiki.”

FAMILIA YA RAIS YAHUSIKA

Yanga wanajua kulinda chao na katika kumtuliza mshambuliaji huyo, kigogo mmoja wa klabu hiyo amefanya akili moja wakimtuma mtoto mmoja wa Rais mstaafu wa nchi hiyo (jina tunalo) kumtuliza mshambuliaji huyo.

Mozizi ambaye amekuwa mmoja kati ya wafungaji bora msimu huu nchini humo akiitumikia klabu yake ya FC Lupopo amefichua kwamba mmoja wa watoto wa rais huyo mstaafu aliyepo kwenye timu hiyo alimfuata na kumtaka atulie na kwamba kama kuna klabu ya kuichezea Tanzania atakwenda Yanga.

“Alikuja yule mtoto wa Rais nilishtuka sana alikuja na magari kabambe (ya kisasa) akaniambia ameagizwa na bosi wa Yanga kwamba natakiwa kwenda kuichezea Yanga,” alisema Mozizi na kuongeza;

“Nikamjibu kwamba ndio Yanga wananitaka na Simba akaniambia basi nitulie na timu ninayotakiwa kwenda kuichezea Tanzania ni Yanga na akanipa na pesa ambayo aliniambia ni yangu ya matumizi lakini haihusiani na ishu za usajili. Ilinisisimua sana.”

AITAKA JEZI YA MAKAMBO

Aidha, Mpiana alisema endapo atamalizana na Yanga anataka kutumia jezi namba 19 ambayo iliachwa na Mkongomani mwenzake, Heritier Makambo anayekipiga AC Horoya ya Guinea.

“Napenda kutumia jezi hiyo ni kama jezi yenye bahati kwangu tangu nimeanza kuitumia nimekuwa nafanya mambo makubwa.”

Yanga jana ilicheza mechi yao ya tatu ya kujiandaa na kurejea kwa ligi na kutibuliwa rekodi yake na KMC kwa kuchapwa mabao 3-0. Imeshinda mechi mbili na kupoteza moja.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...