Search This Blog

Monday, June 1, 2020

Mabeste ashitakiwa polisi na aliyekuwa mkewe kisa hiki hapa

Msanii Mabeste ameteka vichwa vya habari vya burudani siku ya leo Juni 1, 2020, baada ya kuitwa kituo cha Polisi Oyster Bay kwa kosa la kumchafua mitandaoni mzazi mwenziye na mkewe wa zamani Lissa.

 Mabeste amesema ameenda kituo cha Polisi na anasubiria hadi atakapopangiwa kwenda tena na kosa ni kumchafua kupitia wimbo wake mpya wa Back Off na kumtangazia kwa watu na kwenye vyombo vya habari kwamba mtoto aliyekuwa naye sasa hivi ni wake.

"Ishu ni kwamba nilikuwa nimeshtakiwa na mzazi mwenzangu kwamba namdhalilisha, nimeenda kusikiliza malalamiko yake ambayo anadai kwamba nimemchafua kwenye mitandao kupitia wimbo wa Back off, kuwa unamlenga yeye katika kumdhalilisha zaidi, kingine ni mtoto wake aliyempata sasa hivi, anadai natangaza kwamba ni wa kwangu kwa hiyo inamletea shida kwenye mahusiano yake" amesema Mabeste.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...