Search This Blog

Sunday, June 21, 2020

Kotei huyoo anatua tena

By MWANDISHI WETU

KIUNGO aliyeng’ara na Simba, James Kotei amechemka kwenye klabu ya FC Slavia Mozyr ya Belarus na kuvunja nayo mkataba.

Kotei amekuwa akihusishwa na Yanga ambapo habari za ndani zinasema kwamba vigogo wa klabu hiyo wameshafanya naye mazungumzo ya awali na huenda akatua na Mburkina Fasso, Yacouba Sogne ambaye pia Yanga wanamtaka.

Mchezaji huyo alijiunga na timu hiyo miezi mitano iliyopita, inasemekana kwamba ameamua kuachana nayo kwa makubaliano ya pande zote mbili baada ya kushindwa hata kupata namba ya kudumu kwenye wale wanaoanzia benchi.

Kotei alijiunga na klabu hiyo akitokea Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini ambako alishindwa pia kutamba licha ya kusajiliwa kwa mbwembwe.

Katika mechi 13 za klabu hiyo ya Belarus, Kotei hakuanza hata moja huku akiambulia kukaa benchi michezo mitatu tu jambo ambalo lilimchomsha akaomba kusitisha mkataba.

Kama Yanga watakuwa siriazi na mchezaji huyo huenda wakampata kwa bei chee huku ikidaiwa kwamba anaipa Simba nafasi kubwa kwavile amekaa nao kipindi kirefu.

Advertisement

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...