Search This Blog
Wednesday, June 17, 2020
Kauli ya Basata baada ya kuruhusiwa shughuli
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), wametoa shukrani za dhati kwa Rais Magufuli kwa kurejesha shughuli za kisanaa kama ilivyokuwa awali, baada ya kuzuiliwa kwa muda kutokana na janga la Corona.
Akithibitisha hilo Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza amesema, walikuwa wamekaa vikao na wadau wote wa sanaa ili kujadili jinsi gani watafanya shughuli hizo licha ya uwepo wa ugonjwa wa Corona.
"Tayari tulikuwa tumekaa vikao na wadau wote wa sanaa siku ya Mei 28 ili kuangalia ni namna gani ambavyo tunaweza kufanya kazi zetu huku tunaishi na Corona, tulichukua yale maoni na tukapeleka Wizarani, ndiyo maana Rais mwenyewe alitoa tamko ili kurejesha shughuli za michezo, sanaa na burudani, na sisi kama BASATA tumetoa ruksa, lakini haina maana wasanii wavunje sheria na kanuni" Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment