Search This Blog

Sunday, June 28, 2020

Bei ya ufuta ngoma mbichi, wakulima wasema migomo sasa basi

Na Ahmad Mmow, Lindi.

 Bei za ufuta katika chama kikuu cha RUNALI imeendelea kusimama. Kwani katika mnada watatu kwa msimu huu wa 2020 bei ya juu ya mnada wa pili imeshuka.

Wakati bei ya chini ya mnada wa tatu imepanda ikilingashwa na bei ya mnada huo wa pili uliofanyika wilayani Ruangwa . Katika mnada wa leo uliofanyika katika kijiji cha Songambele, wilayani  Nachingwea bei ya juu ni shilingi 1,580 na bei ya chini ni shilingi 1,562 kwakila kilo moja.

Bei ambazo ni tofauti na bei za mnada wa pili ambazo zilikuwa shilingi 1,615 na 1,555. Katika mnada huo wa leo kilo zote 3,481,845 zimenunuliwa na kampuni za  RBST, SM Holding, Mujibu Shamba, HS Impex na Afrisian.

 Mmoja wa wakulima waliozungumza kwenye mnada huo, Haji Nanjase ambaye alizungumza  baada ya mwenyekiti wa RUNALI, Hassan Mpako kuwauliza wakulima waliohudhuria mnada huo kama walikubali au kukataa kuuza kwa bei hizo alisema kutokana na mwenendo wa bei ya zao hilo msimu huu walikuwa hawana njia nyingine zaidi ya kukubali kuuza.

Hata hivyo licha ya kukubali kuuza kwa bei hizo, Nanjase alisema baada ya kubaini soko la zao hilo siyo zuri na kuna uwezekano wa kuendelea kushuka hawatagomea tena bei.

'' Kwa hali ilivyo,  mwenyekiti wa New Matekwe AMCOS na mkulima kwaniaba ya wenzangu nasema tumekubali kuuza. Lakini pia hatutagoma kuuza, migomo sasa basi,'' alisema Nanjase.

Kwaupande wake mwenyekiti wa RUNALI, Hassan Mpako aliwaasa wakulima watafakari wanapotakiwa kufanya uamuzi wanapoulizwa kama wanakubali au wanakataa kuuza zao hilo kwa bei zinafikiwa na wanunuzi

  Mpako alisema kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia njia za kupata taarifa zimerahisishwa. Kwahiyo wakulima wanajua kinachoendelea kuhusu bei za mazao mbalimbali duniani.

 Alisema kwakuzingatia ukweli huo wanatakiwa kuwa makini wanapofanya uamuzi. Kwani hakuna kinachofichwa.

 Aidha Mpako alitoa wito kwa wakulima wawe makini katika ujazaji taarifa zao. Hasa majina wanayotumia wapopima uzito wa mazao yao na majina yaliyopo kwenye akaunti zao za benki.

 Mwenyekiti huyo wa RUNALI alibainisha kwamba uchanganyaji wa taarifa unasababisha kuchelewa malipo ya wakulima wanaochanganya taarifa zao.

Hali inayosababisha waitupie lawama serikali, vyama vikuu na vyama vya msingi bila sababu.Lakini pia alitoa wito kwa viongozi wa vyama vya msingi waandae taarifa za wakulima mapema baada ya kila mnada  kufanyika.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...