Search This Blog

Sunday, June 28, 2020

BAKWATA Mkoa wa Dodoma wapata viongozi wapya


Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Dodoma limefanya uchaguzi na  kumchagua Japhari Mwanyemba kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza hilo kwa Mkoa wa Dodoma.

Akitangaza matokeo hayo katika uchaguzi huo Jijini Dodoma Mwenyekiti wa uchaguzi huo na Mkurugenzi wa Elimu Bakwata Taifa,Ally Abdallah amemtangaza Mwanyemba kushinda kwa kura zote za ndio ambazo ni 37.

Pia,wajumbe hao wamemchagua,Kakogwe Luambano kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Bakwata anaeuwakilisha Mkoa wa Dodoma.

Vilevile  wamewachagua Masheikhe 10 ambao ni wajumbe wa Baraza la Masheikhe Mkoa  na Wajumbe 10 wa Halmashauri kuu ya Bakwata Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa,Mwenyekiti wa Halmashauri kuu ya Bakwata Mkoa,Mwanyemba ameomba ushirikiano huku akiwataka Masheikhe kuyatumia machinjio kama njia ya kuliongezea mapato Baraza.

"Tunajenga Bakwata mpya tunataka kila kitu kionekane na kinyooke,niwaombe tuliochaguliwa tuwalinde Masheikhe,lakini kubwa tutambue mali zetu,tukusanye mapato,"amesema Mwanyambe.

Aidha amewataka wajumbe wengine waliochaguliwa kufanya kazi kwa kushirikiana ili Baraza hilo liendelee kuwa na sifa bora.

Kwa upande wake,Sheikhe wa Mkoa wa Dodoma,Mustapha Rajabu amewataka viongozi hao waliochaguliwa kubadilika, kujitambua na kuacha kuishi kwa mazoea.

Vilevile,amesema wanatakiwa kuisemea vizuri Serikali ya awamu ya tano akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi Wakuu.

"Rais wetu ametuongoza vizuri na maandiko yanasema waheshimuni na kuwatii wenye Mamlaka,sisi lazima tumtii na kumsemea vizuri Rais wetu,msemeeni vizuri,"amesema.

Kuhusu uchaguzi utakao fanyika baadaye mwezi huu Shekhe Rajabu amesema viongozi wa dini ni wajibu kuomba ili wapatikane viongozi wazuri na wanaomcha Mungu na kujali wananchi.

Akitoa neno la shukrani,mara baada ya kuchaguliwa,Mjumbe wa Halmashauri kuu Bakwata anaeuwakilisha Mkoa wa Dodoma,Luambano amesema,Makatibu,Masheikhe na Wenyeviti wote kuifuata Katiba ya Baraza hilo kwani kwa kufanya hivyo mambo yataenda vizuri na hakutakuwa na malalamiko.

Naye,Mwakilishi wa Baraza la Masheikhe Mkoa wa Dodoma,Sheikhe Saidi Rajabu akitoa neno la shukrani amewataka viongozi wenzake wa dini kwenda kufanya kazi kwa kumuogopa Mwenyezimungu.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...